Duration 1:1

WADAIWA SUGU WAPEWA SIKU 90

51 watched
0
0
Published 20 May 2021

#ujenzi #construction #nyumba Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imezipa miezi mitatu Halmashauri za Miji na Wilaya nchini zinazodaiwa deni la jumla ya shilingi bilioni 2.7 na Shirika la Nyumba la Taia kulipa deni hilo baada ya kuingia mkataba wa kujengewa na kuuziwa nyumba. Akizungumza kwenye majumuisho baada ya kutembelea nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Momba mkoani Songwe zilizojengwa na NHC, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk. Aloyce Kwezi amezitaka halmashauri hizo kulipa deni hilo kabla ya Juni 30 mwaka huu. "Tunalipongeza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa kuweza kutekeleza wajibu wake kujenga nyumba mpaka katika halmashauri za pembezoni lakini wanakwamishwa na baadhi ya Halmashauri ambazo hazitekelezi masharti ya kimkataba,"alisema. Akizungumzia Halmashauri ya Momba iliyojengewa nyumba na NHC kama mkandarasi aliitaka ikamilishe malipo ya kiasi cha shilingi milioni 384 kabla ya Juni 30 mwaka huu.

Category

Show more

Comments - 0